Misri imemuondoa balozi wake huko Syria. Tukio hilo ni la hivi karibuni kabisa kuchukuliwa hatua za kidiplomasia ikiwa na lengo la kutoa shinikizo kwa Rais Bashar al- Assad kumaliza ukandamizaji wake kwa wapinzani ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu.
Wanaharakati wa Syria wanasema vikosi vya usalama jumamosi vilifyatulia risasi waandamanaji katika mji mkuu wa Damascuss waliokuwa wanashiriki katika maziko ya watu waliouwawa wakati wa maandamano siku moja kabla.
Maelfu ya watu walioshiriki maziko hayo na mashahidi wanasema mwombolezaji mmoja aliuwawa katika shambulizi hilo.
Wakati huohuo waandamanaji wanaoipinga Serikali waliendelea na harakati zao dhidi ya serikali huku kundi kubwa likijitokeza huko Damascus na mji wa Aleppo.