Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 07:57

Misri yamkamata mwandishi wa Al Jazeera 'kwa uchochezi'


Waandishi wa Al Jazeera waliokamatwa Cairo, Misri mwaka 2015 wakiwa mahakamani kusikiliza hukumu yao.
Waandishi wa Al Jazeera waliokamatwa Cairo, Misri mwaka 2015 wakiwa mahakamani kusikiliza hukumu yao.

Waziri wa mambo ya ndani wa Misri amemtaja mwandishi aliyekamatwa ni Mahmoud Hussain, alikamatwa Ijumaa.

Misri imethibitisha kwamba imemkamata mwandishi wa kituo cha televisheni cha Al-Jazeera, shirika la utangazaji ambalo linafadhiliwa kwa kiwango fulani na familia ya Mfalme wa Qatar, Amekamatwa “kwa uchochezi” kwa niaba ya shirika hilo la habari.

Waziri wa mambo ya ndani wa Misri amemtaja mwanahabari huyo kama Mahmoud Hussain, aliyekamatwa Ijumaa kwa tuhuma za uvunjifu wa amani na kueneza habari za uongo.

Al-Jazeera imesema Misri ilimuweka kizuizini Hussain kwa sababu ya “tuhuma za uzushi” baada ya kuwasili Misri kuizuru familia yake na imetaka aachiwe mara moja.

Hii ni moja ya habari mpya katika mtiririko wa jumla ya waandishi wa Al Jazeera ambao wamekamatwa, kitu kinachopelekea wasiwasi mkubwa juu ya uhuru wa waandishi wanaofanya kazi Misri.

Upeo wa ripoti za Al-Jazeera kufuatia mapinduzi ya Misri ya Arab Spring ya mwaka 2011 na pia kupinduliwa kwa rais Mohammed Morsi mwaka 2013 kumekosolewa kwa nguvu zote na serikali ya Misri.

XS
SM
MD
LG