Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:14

Rais Sissi amesema maafisa wa usalama wamewakamata wanaodhaniwa kuhusika na mlipuko


Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry.
Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry.

Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi amethibitisha kwamba mlipua bomu la kujitoa muhanga ndiye alilipua bomu katika kanisa la dhehebu ya Coptic Orthodox jumapili na kuuwa watu 25.

Rais el-Sissi amesema maafisa wa usalama wamewakamata wanaume watatu na mwanamke mmoja wanaodhaniwa wamehusika na mlipuko huo.

Rais huyo alikuwa akizungumza katika ibada ya mazishi kwa waathirika hao.

Hakuna mtu yeyote aliyedai kuhuska na mlipuko huo.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika -VOA kwenye eneo la tukio anasema shambulio hilo limetokea wakati wa ibada ya jumapili asubuhi katika eneo lililokua na wanawake wengi.

XS
SM
MD
LG