Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:25

Milipuko yasababisha taharuki Brazaville na Kinshasa


Picha hii iliyochukuliwa mto Congo mjini Kinshasa, nchini DRC, inaonyesha mlipuko ambao umeutikisa Brazaville mji mkuu wa Jamhuri ya Congo.
Picha hii iliyochukuliwa mto Congo mjini Kinshasa, nchini DRC, inaonyesha mlipuko ambao umeutikisa Brazaville mji mkuu wa Jamhuri ya Congo.

Milipuko kadhaa imeutikisa mji wa Brazaville na Kinshasa nchini DRC.

Mlolongo wa milipuko mizito imeutikisa mji mkuu wa Brazaville katika Jamhuri ya Congo Jumapili alfajiri, na kusababisha taharuku kubwa mjini humo na pia katika mji wa jirani wa Kinshasa ambao uko upande mwingine wa mto Congo.

Wanadiplomasia na maafisa wa serikali wanasema milipuko ilitokea katika ghala ya silaha kwenye eneo karibu na mto Congo kaskazini mwa Brazaville. Walioshuhudia wameripoti kusikia milipuko mitatu.

Bado haijajulikana kitu gani kimesababisha milipuko hiyo au watu wangapi wamejeruhi katika tukio hilo.

Afisa katika ubalozi wa China mjini Brazaville ameliambia shirika la habari la Beijing Xinhua kwamba mfanyakazi mmoja raia wa China ameuawa na watu kadhaa kujeruhiwa.

Afisa huyo Wang Jia amesema wafanyakazi hao ni wa kampuni ya uhandisi ya Beijing Construction huko Jamhuri ya Congo.

Walioshuhudia wamesema milipuko imesababisha moshi mzito hewani, na pia kuvunja madirisha kote katika eneo la mto huko Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

XS
SM
MD
LG