Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 00:46

Mikhiel Gorbachev, rais wa mwisho wa Urusi, aaga dunia akiwa na umri wa miaka 91


Hayati Mikhail Gorbachev
Hayati Mikhail Gorbachev

Mikhail Gorbachev, aliyekuwa rais wa Urusi, ambaye alimaliza vita baridi bila kumwaga damu lakini akashindwa kuzuia kusambaratika kwa Muungano wa Urusi, alifariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 91, maafisa wa hospitali ya Moscow walisema.

Gorbachev, kiongozi wa mwisho wa Urusi, alishiriki pakubwa katika mikataba kati ya Muungano wa Usovieti na Marekani ya kutaka kupunguza silaha, na ushirikiano na madola ya Magharibi ili kuondoa wingu nzito la mgawanyiko wa Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia na kupelekea muungano wa Ujerumani.

Lakini mageuzi yake mapana ya ndani yalisaidia kudhoofisha Umoja wa Kisovieti hadi ikasambaratika, muda ambao Rais Vladimir Putin ameuita "janga kubwa zaidi la kisiasa la kijiografia" la karne ya ishirini.

"Mikhail Gorbachev amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua ugonjwa mbaya na wa muda mrefu," Hospitali Kuu ya Russia ilisema katika taarifa.

Putin alitoa "rambi rambi zake," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliambia shirika la habari la Interfax.

"Kesho atatuma ujumbe wa rambirambi kwa familia na marafiki," alisema. Mnamo mwaka wa 2018, Putin alisema angebadilisha kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti ikiwa angeweza, mashirika ya habari yaliripoti wakati huo.

Viongozi wa dunia walikuwa wameendelea kutuma risal za rambirambi kufuatia kifo cha Gorbachev.

Mkuu wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen alisema Gorbachev amefungua njia kwa Ulaya huru.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, akitoa mfano wa uvamizi wa Putin nchini Ukraine, akisema "kujitolea bila kuchoka kwa Gorbachev kufungua jumuiya ya Sovieti bado ni mfano kwetu sote".

XS
SM
MD
LG