Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:31

Mkakati wa kupambana na kipindupindu Malawi


Ndege ambazo haziendeshwi na rubani (drone) zinazotumika Malawi
Ndege ambazo haziendeshwi na rubani (drone) zinazotumika Malawi

Kipindupindu nchini Malawi kimeua kiasi cha watu wanne tangu Novemba 2017 na watu zaidi ya 200 wameambukizwa ugonjwa huo.

Nchi kadhaa za Afrika zinakabiliana na milipuko ya kipindupindu ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Zambia.

Idara ya Umoja wa Mataifa ya kuhudumia watoto (UNICEF) injaribu kutumia mbinu mpya za kisasa kushughulikia tatizo hili la kipindupindu kwa kutumia ndege ambazo haziendeshwi na rubani (drone) nchini Malawi, utaratibu ambao ulianza kutumika mwaka jana.

Ndege hizo kazi yake mahsusi ni kuchukua picha za maeneo yaliyokumbwa na kipindupindu katika mji mkuu wa Malawi.

Picha hizo zinatoa ramani ambayo hutumika katika mipango ya kuchukua hatua muafaka katika kuzuia ugonjwa huo usisambae zaidi.

Kabla ya kuanzishwa mpango huu wa kisasa, UNICEF ilitumia alama maalum ili kufahamu maeneo yaliyoathiriwa.

Mark Hereward, mkurugenzi msaidizi wa takwimu na uchambuzi katika UNICEF, anaeleza:

“Lakini si muhimu aina hiyo hiyo ya mawasiliano ambayo watu wameona katika kile ambacho kimechapishwa kama hivi. Kama vile hapo ni sokoni, angalia uchafu ulivyo. Unajua wanaweza kulielewa hilo vyema,” amesema Hereward.

Malawi inaendelea kuandikisha kesi mpya za kipindupindu. Ni ugonjwa unaoambukiza ambao unasababisha kuharisha sana na unaweza kuua katika muda wa saa chache kama matibabu hayatolewi haraka. Kipindupindu kinasambaa kwa njia ya chakula ambacho si salama na maji machafu.

Serikali ya Malawi hadi hivi sasa imeziweka wilaya 16 kati ya 28 katika tahadhari ya kipindupindu.

Picha ambazo zimepigwa zimebainisha kuwa kuna matatizo makubwa ya usafi wa vyoo kwenye wilaya hizo.

Sharif Gwira, mshiriki katika utaratibu wa kukusanya takwimu anasema “tumegundua kwamba kuna watu wanakwenda haja kwenye maeneo ya wazi katika sehemu tofauti, na pia kuna vyoo ambavyo vinahitaji kufanyiwa maboresho katika maeneo mengi na maji hayalindwi yasichafuliwe.

UNICEF inasema mafunzo waliyopata wakati wa majaribio ya matumizi ya drone hayatakuwa yanafanyika nchini Malawi peke yake.

Hereward anasema “nchini Malawi, ina bahati ni sehemu ambako majaribio haya mapya ya teknolojia ya drone yamefanya kazi na njia inayotumiwa na drone imekuwa ni muhimu sana. Na ndiyo sababu kwanini naamini itakuwa ni ya kudumu nchini Malawi. Lakini kwa hakika itatumiwa pia katika nchi nyingine.”

Wakati huo huo, kampeni za umma zinaendelea kuhusu usafi ili kuzuia ugongwa wa kipindupindu, na ni mpango wa kawaida, ni sawa na biashara kuchanganya na furaha.

XS
SM
MD
LG