Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, msemaji wa polisi bi Brenda Muridili amesema Jumatatu kwamba polisi waliitwa na wakazi baada ya harufu mbaya kutokea kwenye moja wapo ya nyumba hizo, ambako mwili wa mwanamke ulipatikana.
Ripoti za polisi zinesema kwamba mwili huo ulikuwa na mavazi yanayolingana na yale yaliyoripotiwa ya mtu aliyepotea mapema mwezi huu. Mshukiwa aliyekamatwa anasemekana kuwa mtu wa mwisho kuonekana na mwanamke huyo. Baada ya upekuzi zaidi, polisi waligundua miili mingine 5 nje ya jengo, karibu na eneo la kutupa taka.
Mashuhuda wameiambia mamlaka kwamba baadhi ya wanawake wafanya biashara ya ngono kutoka eneo hilo wamekuwa wakitoweka katika siku za karibuni. Kufikia sasa jina la mshukiwa huyo halijafichuliwa.