Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 05:56

Miili ya wahamiaji yapatikana Mediterranean, karibu na Libya


Picha ya maktaba ikionyesha wahamiaji kwenye bahari ya Mediterranean.
Picha ya maktaba ikionyesha wahamiaji kwenye bahari ya Mediterranean.

Mwili mwingine zaidi umepatikana karibu na ufukwe wa Libya  Jumamosi, siku moja baada ya boti ya Madaktari wasio na Mipaka,MSF, kupata miili 11 kwenye eneo hilo la bahari ya Mediterranean, na kusema kuwa  tayari wamewaokoa zaidi ya watu 160 kutoka kwenye boti za wahamiaji.

Shirika lisilo la kiserikali la Sea Watch kupitia ukurasa wake wa X limesema kuwa ndege yake iliona mwili uliopatikana leo. Umoja wa Mataifa umeorodhesha zaidi ya vifo 20,000 au kutoweka kwa wahamiaji kati kati mwa Mediterranean, tangu 2014, ikiwa njia hatari zaidi kwa wahamiaji ulimwenguni.

Italy imeomba Tunisia na Libya kuongeza juhudi za kuzuia wahamiaji kuanza safari zao hatari kwenye bahari. Pia imekuwa ikizuia opereheni za meli za uokozi ikisema kuwa zinawapa wahamiaji motisha wa kuelelekea Ulaya, suala ambalo limekanushwa.

MSF wamesema kuwa boti yao ya ukozi ya Geo Barents iliokoa wahamiaji 146 kupitia operesheni mbili, na kisha kupata wengine 20 kwenye boti tofauti.

Forum

XS
SM
MD
LG