Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:14

Michuano ya kanda ya Nile ya mpira wa kikapu kutimua vumbi Cairo


Jiji la Cairo Misri ambalo ni mwenyeji wa michuano ya kanda ya Nile ya ligi ya klabu bingwa ya mpira wa kikapu barani Afrika ambapo pichani ni hoteli ya St. Regis na Hilton Cairo World Trade Center.
Jiji la Cairo Misri ambalo ni mwenyeji wa michuano ya kanda ya Nile ya ligi ya klabu bingwa ya mpira wa kikapu barani Afrika ambapo pichani ni hoteli ya St. Regis na Hilton Cairo World Trade Center.

Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (BAL) imetangaza  orodha ya timu sita zitakazochuana katika hatua ya makundi ya ligi hiyo kwenye Uwanja wa Hassan Moustafa Indoor Sports Complex mjini Cairo, Misri, itakayoanza Jumamosi Aprili 9 na kuendelea hadi Jumanne, Aprili. 19.

Timu sita BC Espoir Fukash (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), Cape Town Tigers (Afrika Kusini), Cobra Sport (Sudan Kusini), FAP (Cameroon), Petro de Luanda (Angola) na Zamalek (Misri) kwa pamoja itashirikisha wachezaji 78 kutoka nchi 12 barani Afrika na Marekani.

Katika mechi ya ufunguzi mabingwa watetezi Zamaleck ya Misri watakumbana na Cobra Sport ya Sudan Kusini . Timu nne bora katika michuano hii ya Nile zitaungana na timu nyingine nne zilizofuzu katika kanda ya Sahara ambazo ni REG (Rwanda), US Monastir (Tunisia), AS Salé (Morocco) and S.L.A.C (Guinea) katika michuano ya mtoano au robo fainali zitakayofanyika mjini Kigali Rwanda kuanzia Mei 21 hadi 28.

Kanda hii ya Nile inawakutanisha wachezaji wawili wa NBA Jamel Artis wa Cape Town Tigers ambaye mara ya mwisho aliichezea Orlando Magic na Ike Diogu wa Zamalek ambaye mara ya mwisho aliichezea San Antonio Spurs. Diogu, ambaye aliingia NBA mwaka 2005 aliposhinda ubingwa wa kikapu Afrika 2015 -FIBA AfroBasket championship akiwa na timu ya taifa ya Nigeria na alitajwa mchezaji bora wa michuano hiyo (MVP) katika michuano ya mwaka 2017.

Kila timu katika kanda hii ya Nile ya timu 6 kutoka nchi 6 za Afrika watakuwa na wachezaji 13 na walau 8 ni rai awa nchi za timu wanayocheza na wengine wanne kutoka nchi nyingine. Na pia si zaidi ya wachezaji wawili kwa kila timu kutoka nje ya Afria. Na katika mpango wa kuinua wachezaji NBA imeweka nafasi ya mchezaji mmoja kwa kila timu kuweza kuchukua mchezaji kutoka NBA Academy ya Afrika iliyoko huko Saly, Senegal, hawa ni vijana wadogo wenye umri wa shule ya sekondari.

Kanda ya Nile itakuwa pia na wachezaji 12 wa zamani waliocheza NCAA daraja la kwanza hapa Marekani ikiwa ni pamoja na wachezaji watano waliocheza NBA G League hii ikiwa ni ligi ndogo ya NBA hapa Marekani wachezaji wengi wakifanya vizuri huko ndio wanapata fursa ya kucheza ligi ya NBA.

XS
SM
MD
LG