Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama anaelekea Afrika kusini ambako anaanza ziara yake ya siku tano katika bara hilo akilenga masuala ya vijana na uongozi, elimu, afya na mazoezi.
Mke wa rais wa marekani, barack Obama atawasili katika mji mkuu Pretoria Jumatatu ambapo atakutana na Rais wa Afrika kusini, Jacob Zuma.
Michelle pia anatarajiwa kwenda Johannesburg kutembelea taasisi ya Mandela pamoja na pia makumbusho ya ubaguzi mjini humo.
Bibi Obama atahutubia kwenye mkutano wa wanawake vijana kutoka nchini za Afrika zilizo chini ya jangwa la Sahara zilizohusika katika juhudi za jamii na uchumi katika nchi zao. Mkutano huo umefadhili na Marekani.
Michelle pia atakutana na mchungaji Desmond Tutu na mashirika yanayopambana na HIV na ukimwi nchini Afrika kusini.
Bibi Obama atakamilisha safari yake kwa ziara ya siku mbili nchini Botswana. Mke wa Rais ameongozana na mama yake mzazi na watoto wake wa kike, Malia na Sasha.