Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:15

Miaka 55 ya uhuru wa Kenya ufisadi bado tatizo:Kenyatta


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Wakenya wanaelezea matumaini makubwa ya nchi yao wakati taifa hilo lilipoadhimisha miaka 55 ya uhuru huku rais wa taifa hilo la Afrika Mashariki, Uhuru Kenyatta, akizitaka idara kuu za serikali kuziba mianya ya kunawiri kwa ufisadi. Kenyatta alieleza kujitolea kupambana na jinamizi hilo kwa mara nyingine baada ya serikali yake kuweka maafikiano na serikali ya Jersey kurejesha nchini humo fedha zinazofungamana na ufisadi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:11 0:00

Katika uwanja wa michezo wa Nyayo jijini Nairobi, wakenya walifurika kusherehekea na kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa nyimbo za kizalendo walielezea kuwa na fahari na matumaini makubwa ya mafanikio ya taifa lao.

Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya

Rais Kenyatta alitumia nafasi hii kuelezea yaliyo moyoni kuhusu kadhia za ufisadi. Kwa muda sasa jinamizi la ufisadi limeonekana kuibuka mara kwa mara kwenye taasisi kuu za serikali ya Kenya, maafisa kadhaa wa kadhaa wakifikishwa mahakamani kushtakiwa huku wengine wengi wakiachiliwa kwa dhamana. Na japo mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji amekuwa akisisitiza kuwa katika kesi hizo upo ushahidi wa kutosha, bado hawapo maafisa wowote waliohukumiwa kutokana na kamata kamata hizi ambazo zimekuwa ibada nchini Kenya.

Mpaka sasa maafisa wengi mno kutoka mashirika ya serikali kama vile shirika la kusambaza umeme, shirika la bima ya afya, shirika la mafuta, shirika la nafaka na mazao, shirika la ustawi wa vijana wanaotoa huduma kwa taifa, wizara ya kilimo, wizara ya misitu, wizara ya Ardhi miongoni mwa taasisi nyinginezo wameshtakiwa kwa makosa ya kukiuka mfumo wa utoaji zabuni na vile vile kutumia madaraka yao kujigawidi mali ya umma.

XS
SM
MD
LG