Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:14

Mgomo nchini Israel umevuruga huduma za usafiri wa umma, na mahospitali


Mgomo unaoendelea nchini Israel kufuatia mateka sita waliopatikana wamekufa huko Gaza
Mgomo unaoendelea nchini Israel kufuatia mateka sita waliopatikana wamekufa huko Gaza

Hatuwezi kupuuza vilio vya watoto wetu ambao wanauawa katika maeneo mitaro ya chini ya ardhi huko Gaza, anasema Bar-David

Mgomo nchini Israel umevuruga huduma katika mabenki, usafiri wa umma, mahospitali, maduka, na uwanja mkuu wa ndege wa nchi hiyo wakati muungano mkubwa wa wafanyakazi wa Israel, ukiishinikiza serikali kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas, siku chache baada ya mateka wengine sita walipopatikana wakiwa wamekufa huko Gaza.

Arnon Bar-David, mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi Histadrut, alisema Jumapili kwamba kufikia makubaliano ya kuwaachilia huru mateka wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza “ni jambo muhimu sana”. “Hadi sasa nimeonyesha uwajibikaji mkubwa, na haikuwa rahisi,” Bar-David alisema.

Lakini nahisi kwamba hatuwezi kukaa bila ya kufanya chochote. Hatuwezi kupuuza vilio vya watoto wetu ambao wanauawa katika maeneo mitaro ya chini ya ardhi huko Gaza; jambo lisiloelezeka. Tuko katika hali inayoendelea kuwa mbaya Zaidi, na tunaendelea kupokea maiti.”

Forum

XS
SM
MD
LG