Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 12, 2024 Local time: 21:00

Mgogoro wa kibinadamu Sudan unazidisha magonjwa ya kuambukiza


Picha ya Mama na watoto wake wakiwa kwenye moja ya kambi wanazoishi watu waliokoseshwa makaazi nchini Sudan. March 20, 2024
Picha ya Mama na watoto wake wakiwa kwenye moja ya kambi wanazoishi watu waliokoseshwa makaazi nchini Sudan. March 20, 2024

Afisa wa WHO amesema kesi 11,327 za kipindupindu zimeripotiwa pamoja na vifo 316 na huwenda idadi hiyo ikaongezeka.

Mgogoro wa kibinadamu kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan pia unazidisha maambukizi ikiwemo kipindupindu na magonjwa mengine yanayosababishwa na bakteria yameua zaidi ya watu 300 katika eneo hilo, afisa mmoja wa shirika la afya duniani alisema leo Ijumaa.

Afisa huyo wa WHO, Margaret Harris amesema katika mazungumzo na vyombo vya habari kwamba kuna kesi 11,327 za kipindupindu huku vifo 316 viliripotiwa na kwamba homa za msimu au Dengue, pamoja na maambukizi ya homa ya uti wa mgongo pia yaliongezeka. “Tunatarajia kuwa na kesi zaidi ya hizi zilizoripotiwa”, aliongeza.

Forum

XS
SM
MD
LG