Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:14

Mganda Victor Ochen ateuliwa katika tuzo ya amani


Victor Ochen
Victor Ochen

Victor Ochen, kijana mwenye umri wa miaka 33 raia wa Uganda ni miongoni wa watu walioteuliwa kwenye tuzo ya amani duniani ya Nobel mwaka 2015. Victor Ochen aliingia katika historia duniani ya kuwa mwanaharakati mdogo kuwahi kuteuliwa kwa tuzo ya Amani ambapo katika maisha yake ya utotoni alishuhudia matukio yaliyotekelezwa na kundi la waasi la Lord’s Resistance Army-LRA la nchini Uganda. Kundi hilo liliwaandikisha watoto kupigana vita, waliwakata watu midomo, pua na masikio.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:56 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

“ Niliwaona wenzangu wenye umri wa chini ya miaka 12 wakichukuliwa na mimi nilikuwa na umri wa miaka 14 nikaunda chama cha Amani ndani ya kambi tuliyokuwa tukiishi. Lengo kubwa lilikuwa ni kusambaratisha uandikishaji wa watoto na waasi wa LRA. Nia kuu ilikuwa ni kuwaleta pamoja na kuwaeleza kwamba kweli tulikuwa tunateseka lakini tusingetengeneza mazingira yatakayotuletea matatizo na machungu zaidi”.

Wapiganaji watoto wa LRA
Wapiganaji watoto wa LRA

Harakati zake za kutafuta amani zilianza akiwa na umri wa miaka 14 pale alipoanzisha kikundi cha amani kwenye kambi aliyopo ili kuwahimiza vijana kuweza kuwazuia waasi wa kundi la LRA ikiwa ni pamoja na kuhubiri Amani kupitia kundi lake la African Youth Initiative Network.

Kijana Ochen aliwahimiza vijana wenzake kutoishi maisha ya kushika bunduki. Alisema kuwa vijana wengi waliuwawa katika vita na hivyo basi anajaribu kuwasaidia watu wanaoishi katika maisha ya vita. “Chaguo langu la amani ndio watu wa jamii yangu wanataka na ninafuraha kubwa kwamba idadi kubwa ya vijana wanahimiza amani”.

XS
SM
MD
LG