Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 09:03

Mfalme wa Morocco amualika Rais wa Ufaransa, Macron


Mfalme Mohammed wa sita wa Morocco, amemwalika Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron kwa ziara rasmi, baada ya Paris kutangaza msimamo wa kuunga mkono mamlaka ya dola la Morocco katika eneo lenye mvutano la Sahara Magharibi. 

Mwaliko huo ulikuwa kwa njia ya barua kutoka kwa mfalme kwenda Rais Macron, akikaribisha uungaji mkono wa wazi wa Paris kwa mamlaka ya Morocco juu ya eneo hilo lenye mvutano.

Mzozo wa Sahara Magharibi, ulioanzia mwaka 1975, ni kati ya Morocco, ambayo inachukulia eneo hilo kuwa ni himaya yake dhidi ya Polisario Front inayoungwa mkono na Algeria, ambayo inapambania uhuru wa eneo hilo kama taifa.

Macron alituma barua kwa mfalme wa Morocco, Jumanne akitambua mpango wa kujitawala wa Morocco kama msingi pekee wa kufikia suluhu ya kisiasa kwa mzozo huo, huku akizingatia sasa na mustakabali wa Sahara Magharibi ndani ya mfumo wa mamlaka ya Morocco.

Mfalme wa Morocco amesema nchi zetu mbili zitashirikiana kufikia suluhu ambayo, ndani ya mfumo wa Umoja wa Mataifa, inaheshimu kikamilifu mamlaka ya Morocco juu ya Sahara yake.

Ameongeza kuwa nchi hizo mbili ziko tayari kukuza ushirikiano wao katika sekta muhimu za kimkakati.

Polisario na Algeria zote zililaani msimamo wa Ufaransa, huku Algeria ikimuondoa balozi wake jijini Paris, katika kujibu msimamo uliotolewa na Paris.

Forum

XS
SM
MD
LG