Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:25

Mfalme al-Sabah wa Kuwait afariki akiwa na miaka 91


Sheikh Sabah al-Ahmad al-Jaber al-Sabah, mfalme wa Kuwait amefariki dunia
Sheikh Sabah al-Ahmad al-Jaber al-Sabah, mfalme wa Kuwait amefariki dunia

Kifo chake kinaacha pengo kwa umoja wa nchi za kiarabu ya Ghuba ya Uajemi inayoshirikiana na chi za Magharibi, kuwa bila ya mmoja wa viongozi wake wazee wenye uzoefu wakati washirika wa kikanda pamoja na Qatar, Saudi Arabia na Misri wamegawanyika na uhasama ambao mfalme Sabah alijaribu kuupatanisha

Mfalme wa Kuwait, Sheikh Sabah al-Ahmad al-Jaber al-Sabah, ambaye alitumia ushawishi wake kama mwanadiplomasia wa juu wa nchi hiyo kusaidia kuunda vita vilivyoongozwa na Marekani dhidi ya wavamizi wa Iraq mwaka 1991 na kisha kama mtawala alisimamia kurejeshwa kwa uhusiano na Baghdad baada ya kuanguka kwa utawala wa Saddam Hussein, amefariki akiwa na umri wa miaka 91.

Televisheni ya serikali ya Kuwait iliripoti kifo hicho lakini haikutoa Habari zaidi. Alikuwa ameripotiwa kupata matibabu nchini Marekani katika kipindi cha msimu wa majira ya joto.

Sabah alikuwa sehemu ya nasaba ya utawala iliyoanza zaidi ya miaka 250. Kifo chake kinaacha pengo kwa umoja wa nchi za kiarabu ya Ghuba ya Uajemi inayoshirikiana na Magharibi, kuwa bila ya mmoja wa viongozi wake wazee wenye uzoefu wakati ambapo wanachama wa kambi hiyo pamoja na Qatar, Saudi Arabia na Misri wamegawanyika sana na uhasama ambao Emir wa Kuwait alijaribu kuupatanisha.

Kabla ya kua mfalme 2006, Shiekh Sabah alikua waziri wa mambo ya kigeni kwa miaka 50 na kuleta uwiyano katika uhusiano na majirani wakubwa wa Kuwait.

Mwana mfalme Sheikh Nawaf al-Sabah, kakake wa kambo ndio anatarajiwa kuchukua nafasi ya uwongozi, katika wakati Kuwait inakabiliwa na tatizo kubwa la fedha kutokana na kupunguka bei za mafuta na athari za janga la virusi via corona.

XS
SM
MD
LG