Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 09:38

Meli zimeanza kuondoka Ukraine zikiwa zimebeba nafaka


Mali ya kubeba mizigo ya Polarnet, ikipakua nafaka baada ya kuwasili Izmit, Uturuki Monday Aug 8 2022. PICHA: AP
Mali ya kubeba mizigo ya Polarnet, ikipakua nafaka baada ya kuwasili Izmit, Uturuki Monday Aug 8 2022. PICHA: AP

Meli mbili zaidi zimeondoka bandari ya Black Sea nchini Ukraine, zikiwa zimebeba mahindi, maharage ya Soya na nafaka nyingine.

Uturuki na Ukraine zimesema kwamba kufikia sasa, meli 10 zimeondoka Ukraine zikiwa zimebeba nafaka kuelekea soko la kimataifa.

Umaoja wa mataifa na Uturuki, walisimamia mazungumzo yaliyopatikana maelewano ya kusafirisha nafaka kutoka bandari za Ukraine, baada ya kutolewa tahadhari kwamba uvamizi wa Russia nchini Ukraine ulikuwa unasababisha uhaba mkubwa wa chakula kote duniani.

Meli ya Sacura, imeondoka bandari ya Pinvdennyi, ikiwa imebeba tani 11,000 za maharagwe ya Soya kuelekea Italy.

Meli ya Arizona nayo imeondoka bandari ya Chornomorsk, ikiwa imebebea tani 48,458 za mahindi kuelekea Iskenderun kusini mwa Uturuki.

Meli ya Polarnet, iliondoka Ukraine Ijumuaa imewasili Derince, kaskazini magharibi mwa Uturuki na nafaka imeanza kupakuliwa.

Kufikia sasa, tani 243 za nafaka zimeondoka kwenye bandari za Ukraine.

XS
SM
MD
LG