Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi aliapishwa upya Jumatatu kwa muhula mwingine wa miaka mitano wakati wa ufunguzi rasmi wa bunge.
Waziri mkuu huyo anatarajiwa kuanza muhula wake kwa kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
Na kwa maneno hayo yaliyotamkwa na spika wa bunge Abdullah Gemeda kupitia mkalimani, Bw. Meles alianza muhula wake wa nne madarakani. Atakapomaliza muda wake wa miaka mitano madarakani, kiongozi huyo ambaye zamani alikuwa kiongozi wa wanamgambo wa kimaxist, atakuwa ametimiza takriban robo karne madarakani.
Chama cha Bw. Zenawi EPRDF na washirika wake kinadhibiti viti 545 kati ya viti 547 bungeni, ukilinganisha na bunge la awali, ambapo kulikuwa na zaidi ya wanachama 150 wa upinzani. Kiti kimoja kinashikiliwa na mgombea wa chama huru na kiti kingine na Girma Seifu, ambaye pekee alikuwa mshindi wa chama cha Medrek Front.