Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:48

Mchungaji Shepherd Bushiri akamatwa baada ya kukimbia Afrika Kusini.


FILE - Pastor Shepherd Bushiri, right, from the Enlightened Christian Gathering stands on stage while his wife speaks to worshippers at the FNB Stadium in Soweto, Jan. 1, 2020.
FILE - Pastor Shepherd Bushiri, right, from the Enlightened Christian Gathering stands on stage while his wife speaks to worshippers at the FNB Stadium in Soweto, Jan. 1, 2020.

Mchungaji aliyejitangaza kuwa nabii na kiongozi wa kanisa. Shepherd Bushiri amejisalimisha kwa polisi nchini Malawi alikokuwa amekimbilia. Bushiri anatafutwa kwa tuhuma za wizi na biashara haramu ya mzunguko wa fedha nchini Afrika Kusini.

Bushiri na mkewe, Mary, walitoroka Afrika Kusini kwenda Malawi wiki iliyopita, wakikiuka masharti ya dhamana ambayo yalikuwa yamewekwa baada ya kukamatwa kwa kuhusika na kesi ya utakatishaji wa mamilioni ya fedha. Bushiri alijisalimisha polisi Jumatano mjini Lilongwe. Msemaji wa polisi James Kadadzera alisema kukamatwa kwake ni kwa kuitikia wito wa hati ya kukamatwa iliyotolewa na shirika la polisi la kimataifa la Interpol.

“Na kwa kweli ilielezwa kwamba wawili hao wanashtakiwa nchini Afrika Kusini na wanaaminika kukiukia masharti ya dhamana yao.” Alisema Kadzera “ kwa hivyo, tulianzisha msako jana, na tuna hakika kwamba wenza hao walipata habari kwamba polisi wanawatafuta, na sasa tunao chini ya ulinzi.”

Kadadzera alisema polisi walikuwa wakichukua taarifa kutoka kwao lakini hawakujua ni lini watafikishwa mahakamani.

Bushiri ni nabii aliyejitangaza mwenyewe na kiongozi wa Kanisa lake la Enlightened Christian Gathering ambalo linadai kuwa na matawi zaidi ya 70 ulimwenguni.

Nchini Afrika Kusini yeye, mkewe na wengine wawili wanatuhumiwa kuiba dola milioni 6.6 kupitia biashara haramu ya mzunguko wa fedha, na wizi.

Msemaji wa Bushiri, Ephraim Nyondo, alielezea sababu ya Bushiri kukimbilia Malawi.

Kile nabii anachotaka ni hukumu ya haki nchini Afrika Kusini. Kumekuwa hakuna dalili ya yeye kuwa na kesi ya haki nchini hum.” Alisema Nyondo.

Kutoroka kwa Bushiri kuliambatana na ziara rasmi ya Rais Lazarus Chakwera nchini Afrika Kusini wiki iliyopita, ambayo ilichochea tuhuma kwamba rais huyo alikuwa sehemu ya mpango wa kuondoka kwa Bushiri.

Hii ilisababisha mzozo wa kidiplomasia wakati ndege ya Chakwera ilipozuiliwa katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Waterkloof Ijumaa, siku hiyo hiyo ambayo Bushiri na mkewe walishindwa kuripoti kituo cha Polisi kwa dhamana.

Sheriff Kaisi ni mhadhiri wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Blantyre.

Aliiambia VOA kwamba kukamatwa kwa Bushiri kunapasa kumaliza mzozo wa kidiplomasia.

“Hatupaswi kuharibu hilo, ambalo ni kubwa kwa sababu ya mtu mmoja. Alisema Kaisi “kwa sababu Malawi isingefaidika chochote kwa kumlinda, kwa mfano, mtu binafsi na kuweka mfumo wa serikali nzima hatarini.”

Wakati huo huo, kikundi cha haki, Malawi kijulikanacho Malawi Empowerment Movement, kilisema Jumatano kwamba Malawi haipaswi kumrejesha Bushiri na mkewe Afrika Kusini mpaka pale serikali itakapohakikisha watapata kesi ya haki.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG