Mazungumzo ya sudan kaskazini na Kusini yaliyolenga kutatua mzozo wa eneo la Abyei bado yamekwama zaidi ya wiki moja baada ya viongozi kutangaza kuwa wako karibu kufikia makubaliano.
Mazungumzo yataendelea Jumatatu mjini Addis Ababa huku pande hizo mbili za Sudan Kusini na Kaskazini zikijaribu kutatua masuala yaliyobaki kabla ya nchi hiyo kujitenga Julai tisa.
Lakini huku mashauriano yakiendelea, imezuka hofu ya kurejea tena vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Wiki moja iliyopita rais wa Sudan Omar Hassan al- Bashir na kiongozi wa Kusini Salva Kiir walikubaliana kimsingi kuondoa majeshi katika eneo la Abyei lenye utajiri wa mafuta na kuruhusu walinda amani wa Ethiopia kuingia katika eneo hilo.
Makubaliano hayo yalitarajiwa kutiwa saini katika hafla jumamosi usiku.