Mazungumzo yatakayofuata yatawahusisha wajumbe wa Marekani na nchi yingine zenye nguvu duniani.
Shirika la habari la serikali ya Iran IRNA, limeripoti kwamba mazungumzo yataendelea na kushirikisha waandalizi wake.
Marekani ilijiondoa kwenye mkataba wa nuclear na Iran mwaka 2018 wakati wa utawala wa rais Donald Trump, na kuiwekea Iran vikwazo vikali vya kiuchumi.
Iran, ambayo inasisitiza kwamba nguvu zake za nuclear ni kwa ajili ya kuzalisha umeme na wala sio kwa kutengeneza silaha, ilijibu kwa kuendelea kusindika nguzu za nuclear kwa kiwango cha juu ya inavyokubaliwa.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Hossein Amirabdollahian amesema kwamba mkataba wa nguvu za nuclear utazingatia na namna Marekani inataka ujadiliwe na itakavyotilia maanani maslahi ya Iran.
Mazungumzo yasiyokuwa ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani kuhusu mkataba wa nguvu za nuclear mwa mwaka 2015, yalianza alhamisi iliyopita, Vienna.