Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 05:23

Mazungumzo mapya kuanza tena Qatar,kati ya Marekani na Afghanistan


Maafisa wa serikali ya Taliban kwenye picha ya awali.
Maafisa wa serikali ya Taliban kwenye picha ya awali.

Marekani imetetea kufufuliwa tena kwa uhusiano wa kidiplomasia kati yake na utawala wa Taliban ikisema kwamba kutenga taifa hilo hakutasaidia Washington kufikia malengo yake nchini humo.

Mwakilishi maalum wa Marekani kwa ajili ya Afghanistan Thomas West anaongoza ujumbe wa Marekani kwenye kikao cha kwanza kwa njia ya moja moja cha mazungumzo na maafisa wa ngazi ya juu wa Afghanistan, baada ya zaidi ya miezi mitatu, mjini Doha, Qatar.

Marekani ilisitisha mwezi Machi kwa ghafla mazungumzo yaliokuwa yakiendelea, baada ya utawala wa Taliban wenye itikadi kali za kiislamu, kupinga kuruhusu wasichana wa taifa hilo kuendelea na masomo yao ya sekondari. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani ameambia VOA kwamba Marekani inalenga kuendeleza maslahi yake nchini Afghanistan kwenye mazungumzo hayo, yakiwemo,kukabiliana na ugaidi, kuimarisha uchumi pamoja na haki za kibinadamu miongoni mwa mengine.

XS
SM
MD
LG