Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:58

Mazrui apatikana, Abdalla hajulikani alipo Zanzibar


Mwanasiasa wa ACT Wazalendo visiwani Zanzibar Nassor Mazrui
Mwanasiasa wa ACT Wazalendo visiwani Zanzibar Nassor Mazrui

Meneja wa kampeni wa chama cha upinzani cha ACT wazalendo visiwani Zanzibar, amesema kwamba alikuwa ametekwa nyara Jumapili na kutishiwa na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki, huku mgombea ubunge wa chama hicho akiwa bado hajulikani alipo, siku chache kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano Oktoba 28.

Meneja wa kampeni wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo visiwani Zanzibar, amesema kwamba alikuwa ametekwa nyara Jumapili na kutishiwa na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki, huku mgombea ubunge wa chama hicho akiwa bado hajulikani alipo, siku chache kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano Oktoba 28.

Mapema Jumapili, chama cha ACT Wazalendo kilisema kwamba naibu katibu mkuu wake, Nassor Mazrui, na mgombea ubunge Abdalla Ali Abdalla, walikuwa wametekwa nyara na watu wasiojulikana katika matukio mawili tofauti.

Mazrui hata hivyo alijitokeza katika mkutano wa kisiasa baadaye Jumapili na kusema kwamba waliokuwa wamemteka nyara walipiga risasi hewani kabla ya kumlazimisha kuingia kwenye gari lao, na baadaye kumpeleka hadi msituni, na kumwachilia huru.

“Wakati wote walipokuwa wameniteka, walinifunga kitambaa usoni nilikuwa sioni chochote. Walinitishia sana. Baadhi ya watu wamesema kwamba nimepanga kutekwa nyara. Kwa sababu gani nifanye hivyo? Kwa manufaa gani?” amesema Mazrui.

Maafisa wa polisi wa Zanzibar hawajatoa taarifa kuhusu tukio hilo.

Chama cha ACT Wazalendo, ambacho kinataka katiba mpya itakayoifanya Zanzibar “kujitawala kikamilifu” hakijatoa ripoti yoyote kuhusu hatma ya Abdalla Ali Abdalla.

Uchaguzi wa urais, ubunge , wajumbe wa baraza la wawakilishi na viongozi wa serikali za mitaa Tanzania bara na Zanzibar, utafanyika Jumatano wiki ijayo.

Mwaka 2001, ghasia zilitokea Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 35.

Wanasiasa wa upinzani katika uchaguzi wa mwaka huu wamesema kwamba mikutano ya kampeni ya wagombea wao imekuwa ikivurugwa mara kadhaa baada ya wagombea wa nafasi mbalimbali kufungiwa nje ya kinyang’anyiro hicho.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imekanusha shutuma za kuwakandamiza wagombea wa upinzani.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG