Kimbunga hicho, chenye upepo mkali wa kasi ya mpaka kilomita 120 kwa saa, ni tishio kwa Mauritius, kituo cha huduma za hali ya hewa cha kisiwa hicho kimesema
“Wakati kimbunga Freddy kinakaribia. Hali ya dhoruba inaweza ikasababisha mafuriko katika maeneo hatarishi ya pwani, kwa hiyo inashauriwa kuzingatia kutokwenda baharini, kituo hicho kimesema.
Video iliyothibitishwa na shirika la habari la Reuters ilionyesha upepo mkali na mawimbi yakipiga hoteli moja iliyoko ufukweni mwa bahari nchini Mauritius huku maji yakiingia kwenye ukumbi wa hoteli hiyo wakati wageni na wafanyakazi wakitazama.
Mamlaka ya kisiwa cha Madagaska kilichopo takribani kilomita 1,130 magharibi mwa Mauritius kuelekea pwani ya Afrika – imesema maeneo ya mashariki ya Mahanoro na kusini mashariki ya Manakara yanatarajiwa kukumbwa moja kwa moja na kimbunga hicho Jumanne jioni.
Chanzo cha habari hii kinatoka shirika la habari la Reuters