Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 21, 2024 Local time: 12:23

Mauritius imefanya uchaguzi wa bunge


Ramani ya Mauritius na maeneo yaliyo jirani nayo.
Ramani ya Mauritius na maeneo yaliyo jirani nayo.

Nchi hiyo yenye watu milioni 1.3 inajitangaza yenyewe kama kiungo kati ya Afrika na Asia.

Mauritius ilifanya uchaguzi wa bunge leo Jumapili, huku Waziri Mkuu Pravind Kumar Jugnauth na wapinzani wake wakuu wote wanaahidi kukabiliana na mgogoro wa gharama za maisha katika visiwa vya Bahari ya Hindi.

Nchi hiyo yenye watu milioni 1.3 inajitangaza yenyewe kama kiungo kati ya Afrika na Asia, ikipata mapato yake mengi kutoka sekta ya fedha inayostawi katika pwani, ya utalii na nguo. Mauritius pia inapokea msaada kutoka China.

Imetabiri ukuaji wa uchumi wa asilimia 6.5 mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 7.0 mwaka jana, lakini wapiga kura wengi bado hawahisi mafanikio.

Muungano wa Alliance Lepep wa Jugnauth umeahidi kuongeza mshahara wa kima cha chini, kuongeza pensheni, na kupunguza kodi ya ongezeko la thamani kwa baadhi ya bidhaa za msingi.

Inasema itatumia malipo kutoka Uingereza chini ya makubaliano ya Oktoba kwa Uingereza kutoa Visiwa vya Chagos huku ikiendelea kubaki na vituo vya anga vya Diego Garcia vya Marekani na Uingereza.

Forum

XS
SM
MD
LG