Tovuti ya tume ya uchaguzi ilionyesha kundi la wagombea binafsi, karibu wote waliopendekezwa na chama cha Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf, au PTI, wakichukuwa viti 101 katika bunge la chini la wabunge 266.
Walifuatiwa na chama cha Pakistan Muslim League-Nawaz, au PML-N, kinachoongozwa na waziri mkuu mwingine wa zamani, Nawaz Sharif, kikishinda viti 75 na kuwa chama kikubwa zaidi katika bunge, kwa sababu wagombea binafsi wanaoungwa mkono na PTI waligombea katika hadhi ya binafsi.
Chama cha Watu wa Pakistan cha Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani Bilawal Bhutto Zardari, kimekuwa cha tatu kwa kupata viti 54, huku vyama vidogo vya kikanda vikifuata.
Forum