Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:49

Matokeo ya awali Madagascar yaonyesha Rajoelina mshindi wa urais


Mshindi wa uchaguzi wa Madagascar Andry Rajoelina (Kulia) na Mpinzani wake Marc Ravalomanana (kushoto) wakati wa kinyang'anyiro hicho nchini Madagascar Novemba 2018.
Mshindi wa uchaguzi wa Madagascar Andry Rajoelina (Kulia) na Mpinzani wake Marc Ravalomanana (kushoto) wakati wa kinyang'anyiro hicho nchini Madagascar Novemba 2018.

Tume ya uchaguzi ya Madagascar imetangaza matokeo ya awali ya duru ya pili ya uchaguzi ambapo mgombea Andry Rajoelina amepata ushindi wa asilimia 55 za kura akimshinda mpinzani wake Marc Ravalomanana aliyepata asilimia 44.

Rajoelina anarejea madarakani baada ya kumshinda hasimu wake mkuu wa kisiasa Ravalomanana katika duru ya npili iliyokuwa na ushindani mkubwa, lakini ni asilimia 48 tu ya wapiga kura walioshiriki kwa mujibu wa taarifa za tume ya uchaguzi.

Mahakama Kuu ya Madagascar ina siku tisa ya kuidhinisha matokeo hayo ya awali na kumtangaza kuwa mshindi.

Uchaguzi huo unachukuliwa kuwa muhimu kabisa kwa kisiwa hicho kikubwa cha Afrika katika juhudi za kurudisha utulivu wa kisiasa baada ya mvutano, ghasia na maandamano yaliyojiri miezi tisa iliyopita yaliyo sababishwa na rais aliyekuwa madarakani kutaka kuwazuia marais wa zamani kugombania tena kiti cha urais.

Duru zote mbili za uchaguzi zilikumbwa na malalamiko ya wizi wa kura kutoka kwa wagombea mbali mbali na hivi sasa Ravalomanana analalamika kuwepo na ubadhirifu wa kura.

Hata hivyo wajumbe wa Umoja wa Afrika waliokuwa wakiangalia uchaguzi huo wamewapongeza wagombea hao wawili kwa kuendesha kampeni nzuri iliyokuwa na ushindani na kuwapongeza wamadagascar na wanasiasa wote kwa kuendesha kampeni kwa Amani na kueleza kwamba uchaguzi umefanyika kwa Amani na utulivu .

Waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU) nao wamesema hawajashuhudia tatizo lolote la wizi na wanachukulia uchaguzi ulifanyika kwa njia ya haki na uwazi.

Rajoelina mwenye umnri wa miaka 44 aliingia madarakani kwa mara ya kwanza 2014, kufuatia malalamiko ya wananchi waliosaidiwa na jeshi, na kumondowa madarakani Marc Ravalomanana mwenye umri wa miaka 69.

Ravalomanana aliingia madarakani 2002 kutokana na uchaguzi wa kidemokrasia na kuondolewa baada ya miaka 7.

Katika duru ya kwanza ya uchaguzi mwishoni mwa mwezi wa Novemba Rajoelina alipata asilimia 39 za kura na Ravalomanana kujipatia asili mia 35.

XS
SM
MD
LG