Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:11

Mataifa ya kiislamu kupambana na IS


Rais Barack Obama akiwa na Mfalme wa Saudi Arabia.
Rais Barack Obama akiwa na Mfalme wa Saudi Arabia.

Pia kuna mashaka kuhusu mvuto wa Sauidi Arabia na taifa kwa ujumla mfumo wa waislamu wa Sunni ambao wakosoaji wanasema wanachochea harakati kama za kundi la Islamic state

Hali isiyoeleweka imezuka katika miji ya mataifa makubwa ya kiislamu dhidi ya mpango wa Saudi Arabia kuungana na mataifa 34 kupambana na ugaidi.

Wakati mpango huo umepokelewa kwa maelezo yenye mvuto kutoka kwa wajumbe waliopendekeza muungano mpya , kuna maswali yaliyozuka kuhusu ushirikiano huo. Jambo lingine ni uwazi wa jinsi gani mataifa hayo yatahusika kijeshi .

Pia kuna mashaka kuhusu mvuto wa Sauidi Arabia na taifa kwa ujumla mfumo wa waislamu wa Sunni ambao wakosoaji wanasema wanachochea harakati kama za kundi la Islamic state. Saudi arabia ni mjumbe wa ushirikiano wa nchi za magharibi unaoongozwa na Marekani katika kupambana na IS lakini ushirikiano wake umekuwa mdogo.

Kikosi cha Saudi katika maandalizi ya kupambana na ugaidi
Kikosi cha Saudi katika maandalizi ya kupambana na ugaidi

Ushirikiano wa waislamu wa Saudi uliotangazwa Jumanne una lengo la kupambana na ugaidi katika eneo, hiyo ni kwa mujibu wa maafisa wa Saudi ambao hawakutoa maelezo ya kina ni jinsi gani utafanya kazi.

Maafisa wa Marekani na Russia walipata maelezo hayo kwenye taarifa kutoka vyombo vya habari .

Waziri wa mambo ya nje wa Russia anasema katika mkutano na waandishi wa habari na waziri wa mambo ya nje John Kerry mjini Moscow mapema wiki hii kwamba walitarajia kupata maelezo kwa kina kutoka kwa wafadhili wa taratibu hizo.

Lakini bado baadhi ya wajumbe wanasema walishangazwa kuona majina yao kwenye orodha .

Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa mambo ya nje wa Pakistan Aizaz Chundry, amesema ameshangazwa kusoma habari kwamba Saudi Arabia imeitaja Pakistan kama mmoja katika muungano huo.

Msemaji wa ofisi ya mambo ya nje Qazi Khalil Ullah, amesema nchi yake bado haijaamua kama inataka kujiunga na ushirikiano huo. Maafisa wa Pakistan tayari wamethibitisha kwenye vyombo kadhaa vya habari kwamba sera ya Islamabad siyo kupeleka kikosi nje ya nchi isipokuwa kwa Umoja wa Mataifa tu.

Wakati huo huo Indonesia ambayo ni nchi kubwa ya kiislamu imesema ilishangazwa na hatua hiyo ya Saudi Arabia na kwamba nchi hiyo bado haifahamu mchango wake ndani yamuungano wa mataifa hayo.

Huko Afghanistan maafisa wamekaribisha kuundwa kwa muungano huo wa kupambana na ugaidi na msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo alisema Jumatano kwamba nchi ilikuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi ikiwemo mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya IS.

Uturuki na Misri nazo zimo katika muungano huo.

XS
SM
MD
LG