Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:49

Nchi za Afrika zatakiwa kuhakikisha ipo amani Sudan Kusini


Ramani ya Sudan Kusini
Ramani ya Sudan Kusini

Mataifa ya Afrika yanayosimamia juhudi za kuleta amani nchini Sudan Kusini yametakiwa yasipoteze fursa mpya ya kushinikiza juhudi  za kumaliza vita nchini humo, mkuu wa timu ya kimataifa inayoangalia usitishaji mapigano amesema Jumamosi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Festus Mogae, rais wa zamani wa Botswana ambaye anaongoza kamati ya pamoja inayoangalia na kutathmini migogoro kama ya vita-JMEC aliwasihi wanachama wa mataifa manane ya IGAD kufanya kazi pamoja. Mogae alisema nchi ya Kenya, Uganda, Somalia, Sudan, Djibouti, Eritrea na Ethiopia lazima waendeleze mtazamo wa pamoja, wazungumze kwa sauti moja, na kuwapa changamoto wale ambao wanaingiza maslahi yao katika kutekeleza mkataba wa amani.

Baadhi ya wapatanishi kuhusu amani Sudan Kusini. Jan. 13, 2014.
Baadhi ya wapatanishi kuhusu amani Sudan Kusini. Jan. 13, 2014.

Mzunguko wa kwanza wa mazungumzo ya kufufua mkataba wa amani wa mwaka 2015 ulipelekea usitishaji mapigano mwezi Disemba ambayo yalidumu kwa saa kadhaa kabla ya vyama hasimu kushutumiana kila mmoja kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya maadui na upinzani. Umoja wa Mataifa unaelezea shinikizo la karibuni la amani kama ni “fursa ya mwisho” ya kumaliza miaka minne ya vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sudan Kusini.

Mzunguko wa pili wa mazungumzo unatarajiwa kufanyika Februari tano. Akizungumza kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika unaofanyika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia, Mogae alisema utaratibu ulikuwa na mapungufu na umetoa fursa ambayo haitakiwi kupoteza muda au kufanyiwa mzaha, kwa mujibu wa taarifa ya JMEC.

Makamu Rais wa zamani Riek Machar(L) na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir
Makamu Rais wa zamani Riek Machar(L) na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir

Wachambuzi wanasema maslahi ya kieneo ya wanachama wa IGAD mara kwa mara yanaleta ugumu wa kukamilisha mambo. Sudan Kusini ilitumbukia katika vita mwezi Disemba mwaka 2013 wakati Rais Salva Kiir alipomshutumu naibu wake wa zamani Riek Machar kwa kupanga mapinduzi.

XS
SM
MD
LG