Mataifa ya Afrika yamepinga pendekezo la Marekani la kutaka kanuni za afya za kimataifa kufanyiwa mabadiliko, hatua ambayo wajumbe wanasema inaweza kuzuia kupitisha kwake wakati wa kogamano la kila mwaka la shirika la afya duniani.
Iwapo mataifa ya Afrika yataendelea kupinga pendekezo hilo, huenda mabadiliko muhimu yanayotarajiwa katika mkutano huo yakakosekana kufanyika, na kufifia matumaini kwamba nchi wanachama zinaweza kukubaliana kufanyia mabadiliko yanayoweza kuimarisha kanuni za shirika la afya la umoja wa mataifa, linalojaribu kuwa na jukumu kuu katika kusimamia maswala ya afya duniani.
Kanuni za afya za kimataifa IHR, zinatoa majukumu kwa nchi wanachama wakati kuapotokea majaga.
Marekani imependekeza mabadiliko 13 yanayolenga kutoa mammlaka ya kutuma wataalam katika sehemu ambazo kuna chanzo cha milipuko ya magonjwa, Pamoja na kuundwa kwa kamati za kutekeleza kanuni hizo.