Shambulizi kama lililotokea Jumapili la mauwaji ya halaiki mjini Orlando, Florida limesababisha hali ya mshangao na maswali mingoni mwa watu kuhusu ni hatua gani Serikali inaweza kuchukua kuzuia hilo kutokea tena.
Idara ya ujasusi ya Marekani ilijua kuhusu Omar Mateen alietekeleza shambulizi hilo na hata kumhoji mwaka wa 2013 na 2014. Lakini afisaa kutoka idara hiyo amesema kuwa hawakumpata na hatia yoyote.
Naibu mratibu wa Program inayohusika na misimamo mikali katika chuo kikuu cha George Washington amesema kuwa shirika la FBI litachukua siku kadhaa zijazo kutadhmini ni kwa nini kesi dhidi ya Mateen ilifungwa, na kama ilikuwa hatua mwafaka.
Daniel Pipes, ambae ni rais wa shirika la Middle East Forum, ambalo hutetea haki za wamarekani kwenye eneo la mashariki ya kati amesema ni vigumu kwa mamlaka kufuatilia watu wenye uwezekano wa kuwa magaidi kwa kuwa mara nyingi hwana historia za uhalifu.
Mshambulizi huyo wa Orlando alidai kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State wakati akipigia maafisa wa usalama simu kabla ya kushambulia huku kundi hilo kupitia chombo chake cha habari likidai kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na mpiganaji wao.