Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 07, 2024 Local time: 05:35

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yalaani uamuzi wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe


 Kiongozi wa upinzani Jameson Timba baada ya kuteremka kwenye lori la magereza alipokuwa akiwasili kwa ajili ya maombi ya dhamana katika mahakama ya Harare.
Kiongozi wa upinzani Jameson Timba baada ya kuteremka kwenye lori la magereza alipokuwa akiwasili kwa ajili ya maombi ya dhamana katika mahakama ya Harare.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamelaani uamuzi wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe siku ya Jumatano wa kuunga mkono uamuzi wa mahakama ya chini unaowanyima dhamana kiongozi wa chama cha upinzani na wanaharakati 78, ambao walikamatwa mwezi uliopita.

Jameson Timba, ambaye alichukua wadhifa wa kiongozi wa chama katika Citizens Coalition for Change (CCC) baada ya Nelson Chamisa kujiuzulu mwezi Januari, alitiwa mbaroni pamoja na vijana wengine wa chama hicho mjini Harare kwa kufanya mkutano usio na kibali.

Walishtakiwa kwa kukusanyika kwa nia ya kuendeleza ghasia za umma na kunyimwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi.

Amnesty International Jumatano jioni ilidai kuachiliwa kwao mara moja na kuelezea kuwa kuendelea kwao kufungwa kama muda mrefu na kusiko na msingi.

Forum

XS
SM
MD
LG