Kuwait ambayo ni mpatanishi wa Qatar na mataifa ya Saudi Arabia, Bahrain, Umoja wa falme za kiarabu pamoja na Misri imewasilisha masharti hayo kwa Qatar.
Katika masharti hayo wameitaka Qatar kuvunja uhusiano na nchi ya Iran, kufunga ubalozi wake nchini humo, na pia kufunga kituo cha habari cha Al Jazeera pamoja na vituo shirika.
Taarifa hiyo imesema kuwa masharti mengine ni pamoja na kuvunja uhusiano wowote ule na makundi ya kigaidi yakiwemo ya kikundi cha Muslim Brothehood, Iskamic State, al Qaida pamoja na lile la Hezbollah kutoka Lebanon.
Nchi hizo ambazo zimeiwekea vikwazo Qatar zimeitaka Qatar iondoshe wanajeshi wa Uturuki walioko nchini humo pamoja na kusitisha ushirikiano wa kijeshi na Uturuki.