Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:58

Mashambulizi zaidi Gaza, Marekani inashinikiza kuwepo utulivu


Wapalestina wakikagua uharibifu uliotokea baada ya wanajeshi wa Palestina kuondoka kambi ya wakimbizi ya Jabalia Mei 31, 2024
Wapalestina wakikagua uharibifu uliotokea baada ya wanajeshi wa Palestina kuondoka kambi ya wakimbizi ya Jabalia Mei 31, 2024

Waandishi wa habari na maafisa wa afya wa Palestina wamesema kwamba mashambulizi ya Israel yameua watu 11 huko Gaza usiku wa kuamkia Jumatatu, huku Marekani ikishinikiza utekelezaji wa mpango wa kusitisha vita na kuachiliwa kwa baadhi ya mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas.

Jeshi la Israel limesema kwamba wanajeshi wake wametekeleza mashambulizi 50 dhidi ya wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, huku wanajeshi wake wa ardhini wakiendelea na operesheni katikati mwa Gaza na mji wa kusini wa Rafah.

Jeshi la Israel lilisema kwamba mwili wa mwanamme anayedhaniwa kuwa mmoja kati ya watu waliotekwa nyara na wanamgambo wa Hamas, umepatikana katika jamii karibu na mpaka wa Gaza ambapo wanamgambo wa Hamas walishambulia Oktoba 7. Mwili wa Dolev Yehoud umepatikana Kibbutz Nir Oz na umetambuliwa baada ya vipimo vya kisayansi.

Rais wa Marekani Joe Biden alisema Ijumaa kwamba Israel ilikuwa imekubali mpango wa kusitisha vita kwa awamu tatu na kuachiliwa huru mateka, akitangaza kwamba muda umefika wa kumaliza vita katika Gaza na kwamba kundi la Hamas halina tena uwezo wa kutekeleza mashambulizi ya kiwango kikubwa dhidi ya Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG