Ghala hiyo ilionekana kuwa kilomita chache tu kutoka kwenye nyingine ambayo ilipigwa na ndege zisizo na rubani za Ukraine mapema Jumatano na kujeruhi watu 13 na pia kusababisha moto mkubwa.
Mamlaka nchini Russia leo Jumamosi ilifunga kipande cha kilomita 100 cha barabara kuu na kuwahamisha abiria kutoka kituo cha karibu cha treni baada ya moto huo kusababisha mfululizo wa milipuko.
Machapisho kwenye programu ya kutuma ujumbe Telegram yalisema ghala la makombora lilishambuliwa karibu na mji wa Toropets, katika mkoa wa Tver nchini Russia takriban kilomita 380 kaskazini magharibi mwa Moscow na takriban kilomita 500 kutoka mpaka wa Ukraine.
Picha ambazo hazijathibitishwa zinazosambaa kwenye Telegram zilionyesha moto mkubwa ukipaa angani wakati wa usiku na moshi mwingi kutoka kwenye milipuko.
Forum