Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 20, 2024 Local time: 11:11

Mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani Korea kaskazini


Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un

Korea Kaskazini imedai leo Jumamosi kwamba imegundua mabaki ya mojawapo ya ndege zisizokuwa na rubani kutoka Korea kusini iliyotoka Korea Kusini na kuanguka Pyongyang.

Korea Kaskazini imetoa picha za mabaki hayo ambayo baadhi ya wachambuzi wanasema ni ya Korea kusini.

Korea Kaskazini, yenye silaha za nyuklia ilishutumu Seoul kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani na kusambaza vijikaratasi katika mji mkuu.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Pyongyang amesema maafisa wa usalama wamepata mabaki ya ndege isiyokuwa na rubani wakati wa kutafuta mabaki hayo katika mki mkuu wa Korea kaskazini, Oktoba 13.

Jeshi la Korea kusini lilikanusha madai ya kutuma ndege zisizokuwa na rubani Korea kaskazini.

Katika taarifa fupi, Korea Kusini imesema kwamba hakuna haja ya kuzungumzia madai ya Korea Kaskazini.

Forum

XS
SM
MD
LG