Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 01:37

Mashambulizi ya Israel katika shule moja huko Gaza yaua watu 34


Wapalestina wapata hifadhi katika shule inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, huko Gaza. Picha ya AP
Wapalestina wapata hifadhi katika shule inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, huko Gaza. Picha ya AP

Mashambulizi ya anga ya Israel usiku kucha hadi Jumatano katika shule ya Umoja wa Mataifa inayowahifadhi wakimbizi wa ndani wa Palestina na kwenye nyumba mbili, yaliua watu 34 wakiwemo wanawake na watoto, maafisa waliripoti.

Shambulizi hilo baya la Jumatano alasiri katika shule ya msingi ya wavulana ya Al-Jaouni katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat huko Gaza, yaliua watu 14 na kujeruhi 18.

Jeshi la Israel limesema nia yake ilikuwa kulenga wanamgambo wa Hamas waliokuwa wanapanga mashambulizi kutoka ndani ya shule hiyo.

Maelfu ya Wapalestina waliolazimika kuhama makazi yao kutokana na mashambulizi ya jeshi la Israel na amri ya kuondoka wamekuwa wakiishi ndani ya shule huko Gaza.

Shule ya al-Jaouni, moja ya shule nyingi za Gaza zinazosimamiwa na Umoja wa Mataifa, ilishambuliwa mara kadhaa muda wote huu wa vita, ambavyo vimeingia mwezi wa 12.

Israel mara nyingi hushambulia kwa mabomu shule, ikisema shule hizo zinatumiwa na wanamgambo wa Hamas.

Linalishtumu kundi la Hamas kwa vifo vya raia wakati wa mashambulizi yake, likisema Hamas ina ngome za wapiganaji wake na inaendesha mashambulizi ndani ya mitaa ya makazi yenye watu wengi.

Forum

XS
SM
MD
LG