Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 06, 2024 Local time: 09:36

Mashambulizi ya anga ya Israel yaua watu 60 huko Gaza


Nyumba iliyoharibiwa na shambulizi la Israel katika Ukanda wa Gaza, Julai 16, 2024. Picha ya Reuters
Nyumba iliyoharibiwa na shambulizi la Israel katika Ukanda wa Gaza, Julai 16, 2024. Picha ya Reuters

Mashambulizi ya anga ya Israel yaliua watu 60 katika maeneo ya kusini na katikati mwa Gaza, kulingana na maafisa wa afya katika eneo la Palestina, huku Israel ikitaka kuwatokomeza wanamgambo wa Hamas ambao inawatuhumu kujificha katika maeneo yanayokaliwa na watu wengi.

Jeshi la anga la Israel limeripotiwa kushambulia ngome 40, ikiwemo miundombinu ya kijeshi na majengo yenye vilipuzi.

Hamas imeishtumu Israel kwa kuongeza mashambulizi yake ya hivi karibuni katika juhudi za kudhoofisha mpango wa sitisho la mapigano ambao Marekani imekuwa ikizishinikiza pande zote kuukubali. Israel inasisitiza kwamba mashambulizi hayo ni katika juhudi za kuitokomeza Hamas.

Katika tukio tofauti, maafisa wa Israel Jumanne walitangaza kwamba wataanza kutuma taarifa kwa wanaume wa Kiyahudi wafuasi wa vyama vya mrengo mkali vya Orthodox kupigana katika vita huko Gaza. Walikuwa hawaruhusiwi kupigana hadi pale Mahakama ya Juu ilipochukua uamuzi mwezi Juni.

Serikali ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu inategemea vyama viwili vyenye siasa kali vya Orthodox katika muungano wake.

Uamuzi huo unatarajiwa kusababisha mvutano ndani ya nchi, na maandamano yalifanyika hapo awali wakati serikali ilipojaribu kusajili wanaume wa Kiyahudi wa Orthodox.

Forum

XS
SM
MD
LG