Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:19

Marufuku kuimba 'Utukufu kwa Hong Kong'


Waandamanaji wakiimba wimbo wa 'utukufu kwa Hong Kong' Sept 21, 2019
Waandamanaji wakiimba wimbo wa 'utukufu kwa Hong Kong' Sept 21, 2019

Mahakama ya rufaa ya Hong Kong imeamua kwamba hakuna anayeruhusiwa kuimba au kucheza wimbo wa maandamano mjini humo.

“Glory to Hong Kong” yaani utukufu kwa Hong Kong, ulianza kutumika kama kitambulisho cha waandamanaji wakati wa maandamano ya kuipinga serikali mwaka 20219.

Jaji Jeremy Poon amekubaliana na serikali katika maamuzi yake leo Jumatano, akisema kwamba mtunzi wa wimbo huo alikuwa na dhamira ya kuutumia kama silaha.

Marufuku inahusisha mtu yeyote anayecheza au kusambaza nakala za wimbo huo kwa lengo la kutaka uhuru wa Hong Kong au kuutumia wimbo huo kama wimbo rasmi wa mji wa Hong Kong.

Utukufu kwa Hong Kong umekuwa ukichezwa katika viwanja vya michezo.

Mji wa Hong Kong hauna wimbo wake wa utambulisho na umekuwa ukitumia wimbo wa China bara.

Forum

XS
SM
MD
LG