Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 09:48

Marekani yatoa msaada wa kijeshi wa dola bilioni 1 kwa Ukraine


Msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine, ukipakuliwa ndani ya ndege kwenye uwanja wa kimataifa wa Boryspil nje ya mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Februari 13, 2022. Picha ya Reuters
Msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine, ukipakuliwa ndani ya ndege kwenye uwanja wa kimataifa wa Boryspil nje ya mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Februari 13, 2022. Picha ya Reuters

Wizara ya ulinzi ya Marekani imetangaza msaada wa kijeshi wa dola bilioni 1 kwa Ukraine, ukijumuisha silaha na vifaa vingine inavyoona kwamba vinahitajika tangu uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine kuanza mwezi Februari.

Msaada huo wa hivi karibuni unajumuisha risasi zaidi kwa maroketi yanayorushwa kwenye masafa marefu, makombora 1,000 ya kuzima mashambulizi ya vifaru, zana za kivita na magari ya kivita 50 ya matibabu, waziri mdogo wa ulinzi anayehusika na sera Colin Kahl amewambia waandishi wa habari Jumatatu.

Msaada huo uliotolewa na wizara ya ulinzi umefikia sasa kiwango cha jumla cha dola bilioni 9.8 za msaada wa kijeshi wa Marekani tangu rais Joe Biden aingie madarakani mwaka jana, na dola bilioni 11.8 tangu Russia ilipodhibiti kinyume cha sheria eneo la Crimea mwaka wa 2014.

Kahl amesema kwamba Russia imepata hasara kubwa tangu uvamizi wa Ukraine kuanza mwezi Februari, akikadiria kuwa Jeshi la Ukraine liliteketeza kati ya vifaru 3,000 na 4,000 vya Russia na kuua kati ya wanajeshi 70,000 na 80,000 wa Russia.

XS
SM
MD
LG