Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:09

Marekani yatoa dola milioni 89 kusaidia kutegua mabomu ya ardhini nchini Ukraine


Wafanyakazi wa manispaa wasafisha nje ya jengo lililoharibiwa na makombora ya Russia katika mji wa Mykolaiv, Agosti 2, 2022
Wafanyakazi wa manispaa wasafisha nje ya jengo lililoharibiwa na makombora ya Russia katika mji wa Mykolaiv, Agosti 2, 2022

Marekani inasema itatoa dola milioni 89 kusaidia kutegua mabomu ya ardhini, vilipuzi na vifaa vingine ambavyo havijalipuka vilivyowekwa nchini Ukraine na wanajeshi wa Russia.

Msaada huo ambao umetangazwa Jumanne na wizara ya mambo ya nje, utasaidia kufadhili, kutoa mafunzo, na kuzipa vifaa timu 100 za kutegua mabomu katika mwaka ujao wakati wanakabiliana na kile maafisa wa Marekani wanakielezea kuwa, tatizo kubwa linalokumba kilomita mraba 160,000 za eneo la Ukraine, ikiwemo asilimia 10 ya mashamba ya Ukraine.

“Hii ni changamoto ambayo Ukraine itakabiliana nayo kwa miongo kadhaa,” afisa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe amewambia waandishi wa habari Jumanne.

Afisa huyo amelinganisha matumizi ya Russia ya mabomu ya ardhini na vilipuzi na vifaa vya kutegwa ardhini vinavyotumiwa na makundi ya kigaidi, kama vile Islamic State inayojulikana pia kama ISIS.

XS
SM
MD
LG