Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:48

Marekani yatoa dola milioni 100 kuzisaidia Uturuki na Syria kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi


Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Melvut Cavusoglu na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken wakiwa ndani ya helikopta kuelekea kwenye maeneo yaliyoteketezwa na tetemeko la ardhi, Februari 19, 2023
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Melvut Cavusoglu na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken wakiwa ndani ya helikopta kuelekea kwenye maeneo yaliyoteketezwa na tetemeko la ardhi, Februari 19, 2023

Marekani inatoa dola zingine milioni 100 kama msaada wa kibinadamu kwa Uturuki na Syria kuzisaidia nchi hizo mbili kukabiliana na athari za tetemeko baya la ardhi ambalo limeua zaidi ya watu 46,000 na kuwaacha mamilioni ya wengine bila makazi.

.Msaada huo mpya unajumuisha jumla ya msaada wa Marekani kufikia milioni 185 na utatolewa kwa mashirika ya kimataifa na yasiyo ya kiserikali ambayo yameshiriki katika juhudi za uokoaji na ujenzi.

Waziri wa Marekani wa mambo ya nje Antony Blinken anaitembelea Uturuki kujionea mwenyewe uharibifu baada ya tetemeko lenye kipimo cha 7.8. Amesema msaada huo mpya utasaidia katika ununuzi wa blanketi, vyakula, nguo za joto, mahema na vifaa vya ujenzi wa makazi.

Msaada huo pia utaunga mkono huduma za afya na matibabu, juhudi za maji safi na usafi, na programu zinazounga mkono elimu ya watoto na vijana zilizoathiriwa na tetemeko hilo.

Blinken Jumapili alisafiri kwa helikopta katika baadhi ya maeneo yaliyoteketezwa na tetemeko hilo la ardhi na mwenzake wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu.

Blinken anatarajiwa kukutana na Rais Recep Tayyip Erdogan leo Jumatatu.

XS
SM
MD
LG