Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 16:35

Marekani yataka Israel na Hamas kuikia makubaliano


Marekani Jumanne imesisitiza vikali kwa Israel na Hamas umuhimu wa kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano ya takriban miezi 11 ya Gaza na kuwaachia huru mateka waliosalia ambao wako mikononi mwa Hamas.

Kuna mateka kadhaa wanaendelea kushikiliwa Gaza, na wanasubiri makubaliano ambayo yatawarudisha nyumbani.

“Ni wakati wa kukamilisha mpango huo,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Matthew Miller, amewaambia wanahabari baada ya vikosi vya Israel kuwapata mateka sita mwishoni mwa juma waliokuwa chini Hamas wamekufa kwenye handaki katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza.

Amesema Marekani itafanya kazi katika siku zijazo na wapatanishi Misri na Qatar kuongeza kasi ya makubaliano ya mwisho. Jambo moja kuu la mzozo katika mazungumzo hayo ni kusisitiza kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwamba wanajeshi wa Israel, wabaki kwenye mpaka kati ya Gaza na Misri.

Forum

XS
SM
MD
LG