Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 01:37

Tumesikitishwa na ucheleweshwaji wa uchaguzi Senegal - Marekani


Waandamanaji nchini Senegal
Waandamanaji nchini Senegal

Marekani imesema inasikitishwa sana na hatua zilizochukuliwa za kuchelewesha uchaguzi wa rais wa Februari 25 nchini Senegal, ambazo, inasema  zinakwenda kinyume na utamaduni wa kidemokrasia wa nchi hiyo.

“Tumesikitishwa hasa na taarifa za vyombo vya usalama kuwaondoa kwa nguvu wabunge waliopinga muswada wa kuchelewesha uchaguzi, na hivyo kusababisha kura ya Bunge, ambayo haiwezi kuchukuliwa kuwa halali, kutokana na mazingira ambayo ilifanyika,” taarifa iliyotolewa Jumanne na wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilieleza, na kuongeza kwamba Marekani ingependa kuona senegal ikiendelea na uchaguzi wake wa rais kwa mujibu wa Katiba na sheria za uchaguzi.

“Pia tunatoa wito kwa serikali ya Senegal kurejesha ufikiaji kamili wa mtandao mara moja, na kuhakikisha kwamba uhuru wa kukusanyika na kujieleza kwa amani, ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari, unaheshimiwa kikamilifu. Marekani itaendelea kushirikiana na pande zote na washirika wa kikanda katika siku zijazo,” taarifa hiyo iliongeza.

Forum

XS
SM
MD
LG