Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:30

Marekani yapeleka zaidi ya dozi milioni 110 za chanjo ya COVID duniani


Mfano wa chanjo aina ya Pfizer-BioNTech na Moderna dhidi ya COVID-19
Mfano wa chanjo aina ya Pfizer-BioNTech na Moderna dhidi ya COVID-19

Katika taarifa yake, White House ilisema chanjo nyingi zilisafirishwa kupitia mpango wa COVAX, wa shirika la afya ulimwenguni, lakini pia kupitia ushirikiano wa kikanda kama umoja wa  Afrika na jumuiya ya Caribbean (CARICOM)

White House ilitangaza Jumanne kwamba Marekani imepeleka zaidi ya dozi milioni 110 za chanjo za COVID-19 zilizotengenezwa Marekani, kwa zaidi ya mataifa 60.

Katika taarifa yake, White House ilisema chanjo nyingi zilisafirishwa kupitia mpango wa COVAX, wa shirika la afya ulimwenguni, lakini pia kupitia ushirikiano wa kikanda kama umoja wa Afrika na jumuiya ya Caribbean (CARICOM).

White House ilisema michango hiyo inaonyesha kutimiza ahadi ya Rais Joe Bisden ya kutoa angalau dozi milioni 80 kwa mataifa mengine kote ulimwenguni na dozi ni malipo ya awali yam amia ya mamilioni ya zaidi ya dozi ambazo Marekani itatoa katika wiki zijazo.

Taarifa inasema utawala wa Biden, utaanza kusafirisha dozi nusu bilioni za chanjo ya Pfizer na BioNTech kwa nchi 100 zenye kipato cha chini duniani. Biden anatarajia kujadili michango hiyo na juhudi nyingine, baadae Jumanne.

XS
SM
MD
LG