Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:02

Marekani yampongeza Ruto


Rais mteule wa Kenya William Ruto akihutubia taifa baada ya mahakama ya juu kuidhinisha ushindi wake. Nairobi, Sept. 5, 2022. Picha: Reuters
Rais mteule wa Kenya William Ruto akihutubia taifa baada ya mahakama ya juu kuidhinisha ushindi wake. Nairobi, Sept. 5, 2022. Picha: Reuters

Marekani imetuma ujumbe wa pongezi kwa rais mteule wa Kenya William Ruto, baada ya mahakama ya juu kuidhinisha ushindi wake.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken, amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba anatarajia kwamba ushirikiano kati ya Kenya na Marekani utaimarika chini ya uongozi wa Ruto.

Blinken vile vile amemshukuru mpinzani mkubwa wa Ruto, ambaye ni Raila Odinga kwa kukubali uamuzi wa mahakama.

“Tunampongeza Raila Odinga kwa kukubali uamuzi wa mahakama ya juu. Uchaguzi ulio huru na amani, na hatua ya kufuata mkondo unaofaa kusuluhisha migogoro kupitia kwa taasisi zilizopo ili kukuza demokrasia,” amesema Blinken.

Odinga aliwasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Ruto lakini kesi hiyo imetupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.

Ujumbe wa Uingereza

Waziri wa Uingereza anayehusika na maswala ya Afrika Vicky Ford, amesema kwamba Uingereza inatarajiwa kufanya kazi na Dr. William Ruto ili kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Ford amesema kwamba “Kenya na viongozi wake wameweka mfano mzuri sana kwa ulimwengu kwa jumla kwa kuandaa uchaguzi ulio huru na wazi kabisa.”

Museveni azungumza na Ruto

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameandika ujumbe wa Twitter na kusema kwamba amezungumza na Ruto moja kwa moja na kumtakia kila la heri katika majukumu yake kuiongoza Kenya.

“Nina matumiani mengi kwamba tutashirikiana na Ruto katika kutimiza maslahi ya Jumuiya ya Afrika mMshariki. Mungu aibariki Kenya,” ameandika Museveni.

Ujumbe wa Umoja wa Afrika

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amesema kwamba “anampongeza sana rais mteule wa Kenya William Ruto kama rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya na kumpongeza Raila Odinga kwa kuheshimu maamuzi ya mahakama”.

Naye makamu rais wa Ghana Mahamudu Bawumia amesema, “kila la heri kwa rais mteule wa Kenya William Ruto unapochukua uongozi wa taifa la Kenya tunalolipenda. Mungu akuongoze katika kila hatua unayochukua”.

XS
SM
MD
LG