Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:18

Marekani yampiga marufuku Gen Kayihura wa Uganda


Generali Kayihura (Kulia) asalimiana na Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Generali Kayihura (Kulia) asalimiana na Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Serikali ya Marekani imempiga marufuku aliyekuwa mkuu wa polisi wa Uganda Generali Kale Kayihura, pamoja na familia yake, kuingia Marekani.

Marekani ilisema ina taarifa za kuaminika kwamba Kayihura, ambaye alikuwa mkuu wa polisi wa Uganda kati ya mwaka 2005 na 2018, alihusika katika ukandamizaji wa haki za kibinadamu.

Taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, inasema Generali Kayihura alihusika moja kwa moja katika kuwatesa watu, kufanya ukatili dhidi ya raia wa Uganda, kwa kuunda kikosi maalum katika jeshi la polisi kilichopata amri ya moja kwa moja kutoka kwake na kuwadhulumu raia wa Uganda wakati wa uongozi wake.

Kulingana na sheria za kimataifa za Marekani, wizara ya mambo ya nje ya Marekani inapokuwa na taarifa za kuaminika kuwahusu maafisa katika serikali za nje, wanaojihusisha na vitendo vya ufisadi, au ukandamizaji wa haki za kibinadamu, maafisa hao na watu wa familia zao wanapigwa marfuku kuingia Marekani.

Mke wa Kale Kayihura, Angela Umurisa Gabuka, binti wake Tesi Uwibambe, na mtoto wake wa kiume Kale Rudahigwa, nao pia wamepigwa Marufuku kuingia Marekani.

Serikali ya Marekani imesema hatua dhidi ya Kayihura inatokana na wasiwasi wa kuendelea kwa ukandamizaji wa haki za kibinadamu nchini Uganda na kutaka serikali yake Yoweri Museveni kuheshimu haki za kibinadamu, uhuru wa raia wake na kuwapa uhuru wa kuandaa mikutano ya uma kwa njia ya amani.

-Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Kennes Bwire, Washington DC.

XS
SM
MD
LG