Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 28, 2024 Local time: 18:40

Marekani yaiwekea Iran vikwazo zaidi


Marekani Alhamisi imetangaza vikwazo vipya vinavyoilenga Iran ikijibu kuendelea kuongezeka kwa shughuli za nyuklia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema katika taarifa yake.

“Katika mwezi uliopita, Iran ilitangaza hatua za kupanua zaidi mpango wake wa nyuklia kwa njia ambazo hazina malengo ya amani ya kuaminika,” Waziri Blinken amesema.

“Tunaendelea kujitolea kutoiruhusu Iran kamwe kupata silaha za nyuklia, na tumejiandaa kutumia nguvu zote za kitaifa kufanikisha matokeo hayo.”

Ujumbe wa Iran wa Umoja wa Mataifa, jijini New York haukujibu mara moja ombi la kutoa maoni.

Hatua ya Alhamisi imeweka vikwazo kwa kampuni tatu za Umoja wa Falme za Kiarabu ambazo Marekani inazituhumu kuhusika katika usafirishaji wa mafuta ya Iran au bidhaa za kemikali za petroli, pamoja na meli 11 zinazohusiana kampuni hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG