Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 20:58

Marekani yaitaka Sudan kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Mmarekani


Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Ned Pr
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Ned Pr

Marekani, Alhamisi iliitaka serikali ya Sudan kutumia njia zote za kisheria kubadili uamuzi wa wiki hii wa kumuachilia raia wa Sudan anayekabiliwa na hukumu ya kifo kwa mauaji ya mwanadiplomasia wa Marekani mwaka 2008.

Abdelraouf Abuzeid alipatikana na hatia, pamoja na wengine, katika mauaji ya Mmarekani, John Granville na mwenzake wa Sudan, ambao wote walikuwa wakifanya kazi katika Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani na waliuawa na watu wenye silaha mjini Khartoum.

"Tunatoa wito kwa serikali ya Sudan kutumia njia zote zilizopo za kisheria ili kutengua uamuzi huu na kumkamata tena Abuzeid," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Ned Price aliwaambia waandishi wa habari.

Maafisa walikutana na balozi wa Sudan, Marekani, Alhamisi na balozi wa Marekani, Sudan, John Godfrey, anawashirikisha maafisa wa Sudan katika ngazi za juu kuhusu suala hilo, Price alisema.

XS
SM
MD
LG