Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:24

Marekani yaionya Uganda, Kenya kuhusu Sudan Kusini


Sigal Mandelker, naibu waziri wa Marekani kwa masuala ya ugaidi Afrika
Sigal Mandelker, naibu waziri wa Marekani kwa masuala ya ugaidi Afrika

Naibu waziri wa Marekani anayeshughulika na masuala ya ugaidi na masuala ya ujasusi unaohusiana na fedha, Sigal Mandelker alitoa wito kwa nchi ya Uganda na Kenya kusitisha mmiminiko wa wawekezaji wa Sudan Kusini waliogubikwa na ulaji rushwa ndani ya nchi zao.

Mandelker alisema viongozi wa Uganda na Kenya lazima wakome kuwaruhusu maafisa wa Sudan Kusini kununua mali kwa kutumia utaratibu wa rushwa.

Mandelker, ambaye anatembelea baadhi ya nchi za Afrika wakati huu aliwaambia waandishi wa habari kwenye ubalozi wa Marekani mjini Kampala siku ya Jumatatu kwamba serikali ya Marekani imeweka wazi kwa wabunge wa Uganda na Kenya pamoja na mabenki kwamba ni jukumu lao kuwazuia maafisa wa Sudan Kusini walaji rushwa kuchukua fedha haramu zilizopatikana kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka minne na nusu na kuwekeza fedha katika biashara ya nyumba huko Uganda na Kenya.

XS
SM
MD
LG